Saturday, May 12, 2018

JINSI YA KUFIKIA MALENGO YAKO

SIMULIZI FUPI YA MAISHA YANGU...

   Kwa majina naitwa ISAACK KANYANKOLE,,mzaliwa wa Bukoba napenda kuwashirikisha vijana wenzangu tusitegemee kuwaajiriwa tutegemee kujiajiri wenyewe.

   ..SOMA KWA MAKINI HUKU UKIJIFUNZA ZAIDI..

   Nakumbuka mwaka 2017 nilipata baadhi ya matatizo kwenye familia yangu sikuweza kukata tamaa ilinibidi kujikita rasmi katika tasnia ya uandishi maana niliona wazi ni sehemu ambayo ingeweza kunipatia kipato cha kujikimu mimi na familia yangu.

  Naam ilikuwa hivyo ijapokuwa kwa mara ya kwanza nilipata ugumu fulani juu ya kuuza kazi zangu ila sikuweza kukata tamaa niliendelea kuandika simulizi huku nikiamini hii ndo kazi yangu...ijapokuwa nilikuwa naandika ila kuna baadhi ya watu walikuwa wananunua mwisho wa siku niliweza kupata dili kwenye media fulani huko Bukoba nilifanya nao kazi moja na baada ya kufanya nao kazi moja ilinibidi kuandika simulizi nyingi sana.

   ...Sikuweza kukaa Bukoba kwamaana nilitaka nifanye kazi zangu ziweze kutambulika Tanzania nzima hivyo nilitafuta nauli kupitia kazi hii ya uandishi na baada ya kufanikiwa kupata nauli niliweza kuja Dar es salaam.
   Nilifikia kwa kakaangu nilikaa nae kwa miezi kama miwili na hatimae baada ya kupata pesa kupitia simulizi ilinibidi kupanga chumba changu.
   Ila baada ya kupanga chumba sikuishia hapo maana nilitaka kuwa na ofisi yangu hivyo nilikusanya pesa ambazo nilikuwa napata kupitia simulizi na kuweza kufungua ofisi yangu..

  Kupitia simulizi hii fupi nimetaka kuwaonesha vijana wenzangu kuwa kila kitu kinawezekana ukiamini wewe na hakuna ambaye ana kipaji bali kipaji kinatafutwa na wewe mwenyewe ukiamua.

    Hivyo na wewe napenda uchukue Fursa yako sasa na pia ukiwa unapenda na wewe kuwa mmojawapo wa shabiki zangu unaweza kununua simulizi zangu ambazo nauza whastup,,na hata facebook.

NA PIA MALENGO MENGINE AMBAYO NIKO NAYO MPAKA SASA NI ;
01.KUTOA VITABU
02.KUWA NA APP YANGU
03.KUWA NA ALBUM YA NYIMBO ZANGU

   NATUMAI VYOTE HIVI VITATIMIA KWAMAANA NINAAMINI NINACHOKIFANYA..HIVYO NA WEWE KIJANA MWENZANGU ANZA SASA KWA KUAMINI KUJIAJIRI NA SIO KUAJIRIWA.

  ILA KUMBUKA UKIFANYA JAMBO LOLOTE KWA KUAMINI KUNA WATU WANAONA UNACHOKIFANYA,,USIKATE TAMAA KWA KAULI ZA WAKATISHAJI TAMAA MAANA HAO WAPO ILI WEWE UFIKIE MALENGO YAKO..

SIMULIZI HII YA MAISHA YANGU UTAKUJA KUIPATA MWANZO MWISHO KUPITIA KWENYE KITABU CHANGU HIVYO USIKOSE MAANA KUNA CHANGAMOTO NYINGI AMBAZO NIMEPITIA MPAKA NILIPO SASA...

NA PIA   NAZANI UMEWEZA KUPATA SOMO KUPITIA SIMULIZI YANGU FUPI HIVYO UNAWEZA KUJIPATIA KAZI ZANGU KWA ADA NDOGO SANA ILI UWEZE KUBURUDIKA HUKU UKIJIFUNZA..

  ..KARIBU SASA..

1 comment:

  1. Live Casino Real Money – The Ultimate Guide to Playing
    Live casino 바카라 검증사이트 is an online sports 벳 365 가상 축구 주소 betting service that is 피망 포커 머니 상 There 스포츠토토 is no live casino real money available 일본 야구 분석 사이트 and you may not be able to play real money games in

    ReplyDelete

JINSI YA KUFIKIA MALENGO YAKO

SIMULIZI FUPI YA MAISHA YANGU...    Kwa majina naitwa ISAACK KANYANKOLE,,mzaliwa wa Bukoba napenda kuwashirikisha vijana wenzangu tusitegem...