Thursday, May 10, 2018

CHOMBEZO;KUMBE ALBINO MTAMU 2

'CHOMBEZO YA MAPENZI'

      'INAITWA'

--KUMBE ALBINO MTAMU?.--

MTUNZI;Isaack Kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;02

    ...ILIPOISHIA...

Mmojawapo wa wawindaji hao alinisogelea na kuniuliza jina langu niliweza kumwabia ila baada ya kumwambia jina langu mwanaume huyo aliweza kunisihi nikimbie huku akiwa anajaribu kutazama wenzake ambao walikuwa wanaonekana kunitazama na hatimae wawindaji hao walinisogelea huku wakiwa wanaonekana wazi kuwa na ushari fulani kwa jinsi sura zao zilivyokuwa!?..

     ...ENDELEA...

Na kweli kwa jinsi nilivyokuwa nawakisia ilikuwa hivyo kwa maana wawindaji hao walianza kunikimbiza huku wakiwa wanajaribu kunitisha kwa maneno ya ukali ila sikuweza kusimama nilikimbia mpaka tulipokuwa tunaishi.
   Sikufahamu kama  nilikuwa nimefanya kosa kwamaana niliweza kushuhudia wazazi wangu wakikatwakatwa viungo vyao na watu hao kwa jinsi walivyokuwa wakikata viungo vya wazazi wangu walionekana kushangilia na baada ya watu hao kumaliza kukatakata miili ya wazazi wangu mmoja wa wawindaji aliweza kuwazuia wawindaji hao huku akijaribu kuwazuia kuwa siku nyingine ndo wataweza kufanya dhamira ya kunikatakata.

    Hivyo baada ya wauaji hao kuelezewa na mwanaume huyo ambaye alionekana waziwazi kutokubalina juu ya jambo ambalo walikuwa wamefanya la kuua wazazi wangu.
    Mwanaume huyo aliweza kunifunga kamba na kisha aliweza kunipatia kidonge fulani alinisisitiza kuwa nikimeze na kweli niliweza kumeza kidonge hicho na baada ya kukimeza kidonge sikuelewa ni nini ambacho kiliendelea baada ya kujikuta nikiwa mgongoni mwa mwanaume huyo akiwa anakimbia.

   Na baada ya kuzungumza mwanaume huyo aliweza kunishusha chini na kufurahia ila kipindi akiwa anajaribu kutaka kunisimulia maana mambo ambayo yalikuwa yamenitokea niliona kama yalikuwa kama ndoto ila kwa mbali na sehemu tulipokuwa tuliweza kusikia michakacho ya watu wakiwa wanakuja tulipokuwa mwanaume huyo alinibeba tena mgongoni na kuanza kukimbia ila kipindi akiwa anakimbia aliweza kujikwaa na kudondoka chini na baada ya kudondoka chini mwanaume huyo akuweza kuendelea kukimbia alidai kuwa nikimbie nilijaribu kumsihi lakini hakuweza kunyanyuka hivyo nilimuacha na baada ya kumuacha nilianza kukimbia mpaka nafika katika kijiji chenu.

"Dah,,pole sana inatupasa kukupeleka kwa kiongozi wa kijiji hiki ili uweze kuishi hapa maana kijiji hiki hususani ni kijiji cha watu wakarimu sizani kama mkuu wetu hatakataa". Mwanaume huyo aliongea akiwa anasimama na kunishika mkono.
   Niliongozana nae mpaka kwenye nyumba ambayo ilikuwa imejengwa kwa tofali na pia ilikuwa imeezekwa kwa mabati tulisimama kwa nje, mwanaume ambaye alikuwa amenileta katika sehemu hiyo aliingia ndani hakuchukua muda mwingi alitoka ndani akiwa ameongozana na mwanaume ambaye alionekana wazi kuwa na umri kuanzia miaka kama tisini hivi ila cha ajabu alikuwa anatembea vema tu.

   Kiongozi huyo baada ya kutoka nje aliweza kunitazama usoni kana kwamba anaonekana kunitafakari juu ya jinsi nilivyokuwa na pia mwanaume ambaye alikuwa amenileta katika sehemu hiyo alionekana kumuelezea juu kisa changu.

"Nazani kijiji hiki ni cha ukarimu hivyo nataka ambaye atahishi na huyu kijana?". Kiongozi huyo aliongea akiwa  anasimama mbele ya wanakijiji ambao walikuwa wamezingira katika sehemu hiyo.

Hakuna hata mmoja ambaye aliweza kuzungumza kila mtu alibaki kimya huku wengi wao wakionekana kunishang'aa kwa jinsi nilivyokuwa. "Nitaishi nae mimi". Ilikuwa ni sauti ya mwanaume ambaye alikuwa amenileta katika sehemu hiyo alizungumza akiwa ananisogelea nilipokuwa na kunishika mkono.

Kila mtu aliyekuwa katika sehemu hiyo alipiga makofi na hatimae nilipelekwa kwa kiongozi huyo wa kijiji hicho kiongozi huyo aliongea maneno fulani ambayo sikuelewa alikuwa ana maana gani?, na baada ya kumaliza kuongea aliweza kuniruhusu kusimama.

   Kila mtu aliyekuwa katika sehemu hiyo aliweza kuondoka hivyo na mimi niliongozana na mwanaume huyo nilienda nae mpaka kwake nilioneshwa chumba ambacho ningetumia kulala. Na siku iliyofuata niliamka mapema na kusafisha uwanja na baada ya kumaliza kusafisha uwanja nilienda moja kwa moja mtoni kwamaana niliweza kufahamu ulipokuwa ila baada ya kufika mtoni niliweza kukuta wanaume fulani wakiwa mtoni na walikuwa wameshika mapanga.
   Niliteka maji huku nikiwa natetemeka na baada ya kumaliza kuteka maji nilibeba vifaa vyangu ila kitendo cha kupiga hatua kama mbili hivi wanaume hao walinizunguka huku wakiwa wameweka vidole vyao kinywani mwao kuashilia nisipige kelele.

"Ukijaribu kupiga kelele tunakuua hivyo kaa kimya". Kijana mmoja aliongea huku akiwa ananisogelea nilipokuwa na baada ya kunisogelea nilizibwa na kitambaa usoni sikufahamu kilichoendelea maana baada ya kuniweka kitambaa usoni nilihisi macho yangu kuwa mazito.

   Nilishtuka baada ya kumwagiwa maji na nilipotazama nilipokuwa sikuweza kufahamu ang'arabu niliweza kusikia minong'ono ya watu wakibishana na baada ya watu hao kubishana kwa muda mrefu na mara waliweza kuwasha taa nilipigwa na bumbuwazi baada ya kuona sehemu nilipokuwa kwa jinsi ilivyokuwa inafanana!?...

 


















ITAENDELEA...


















  Usikose kipande hata kimoja cha chombezo hii kali ambayo itakuacha umepata mafunzo mbalimbali...















Na kama ujalike page yangu unachelewa nini like page yangu inayoitwa
STORY ZA KUSISIMUA&MIKASA











'KARIBU'

No comments:

Post a Comment

JINSI YA KUFIKIA MALENGO YAKO

SIMULIZI FUPI YA MAISHA YANGU...    Kwa majina naitwa ISAACK KANYANKOLE,,mzaliwa wa Bukoba napenda kuwashirikisha vijana wenzangu tusitegem...