Thursday, May 10, 2018

CHOMBEZO; KUMBE ALBINO MTAMU

'CHOMBEZO YA MAPENZI'

     'INAITWA'

---KUMBE ALBINO MTAMU?.---

MTUNZI;Isaack Kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;01

     ...UTANGULIZI...

Hii ni chombezo ambayo imesukwa vema hivyo soma kwa umakini huku ukijifunza maana mambo ambayo utakuta katika chombezo hii yatakuacha umepata funzo kubwa sana.. Mtunzi wa chombezo hii anashauri kwa ambaye atasoma chombezo hii awe na umri wa kuanzia miaka 18+ maana kuna mambo ambayo yatakuacha ukiwa hoi taabani,,na pia tuepukane na mila potofu katika jamii ambazo tunaishi. Soma kisha ujifunze.

    ...ANZA NAYO...

  Radi na mingurumo zilisikika kwa mbali sana,,kwamaana nilikuwa nimebebwa mgongoni na mtu aliyekuwa amenibeba alikimbia kwa kasi sana. Hivyo sikuwa nasikia vema mtu huyo aliendelea kukimbia na kila alivyokuwa anakimbia niliweza kukumbuka matukio ambayo yalikuwa yamenitokea kwa muda mfupi uliokuwa umepita.

"Niachie mimi". Nilizungumza kwa ukali sana huku nikijaribu kuleta purukushani za hapa na pale maana nilikuwa nina hofu kubwa sana juu ya mambo ambayo yalikuwa yamenikuta kwa kipindi kifupi.

  Na kweli baada ya kufanya purukushani za hapa na pale mtu huyo aliweza kunishusha huku akiwa anaonekana kutoamini. "Pole sana David". Mtu huyo aliongea akiwa ananitoa mgongoni kwake.

"Mama na baba wako wapi?". Niliuliza huku nikiwa nimemtazama mtu huyo ambaye sikuwa namfahamu.

"Wazazi wako wameuwawa kwa kuchinjwa na mapanga na hapa unatafutwa na watu hao wabaya". Kijana huyo aliongea akiwa  amenitazama usoni kana kwamba anafikiri kwa ambacho nitakifanya.

  Ila kipindi hichohicho kwa mbali tuliweza kusikia watu wakija tulipokuwa hivyo kijana huyo alinibeba tena na kuanza kukimbia ila kipindi akiwa anakimbia na mara aliweza kuteleza na kudondoka.

"David kimbia watu hao ni wabaya watakuua kimbia niache maana siwezi kuendelea na safari nendaaa". Kijana huyo alisinisitiza huku akiwa ameshika mguu wake.

"Amka twende watakuua hao watu?". Nilizungumza nikiwa najaribu kumnyanya kijana huyo lakini alikataa katukatu na kudai asingeweza kuendelea na safari hivyo alinisisitiza niendelee kukimbia.

   Ilinibidi kumuacha kijana huyo na kuendelea kukimbia nilikimbia huku nikiwa nageuka nyuma na kutazama kama watu hao walikuwa wananikimbiza ila sikuweza kumuona mtu yoyote yule ang'arabu niliweza kusikia sauti ya mtu akipiga kelele ya kuomba msaada.

'Ina maana kile ambacho nilikuwa nakiota ni kweli'. Niliwaza nikiwa naendelea kupanda mlima.

  Na baada ya kumaliza kupanda kilele hicho cha mlima kwa mbali na sehemu hiyo niliweza kufanikiwa kuona watu wakiwa wanafanya shughuli za hapa na pale hivyo nilianza kutembea kuelekea katika kijiji hicho nilitembea takribani masaa mawili na jua lilipokuwa kali sana ilinibidi kwenda kwenye kivuli maana nilihisi kuungua kwa ngozi yangu.
Na baada ya jua kuzama niliendelea na safari mpaka kwenye kijiji hicho naam baada ya kufika katika kijiji hicho ila kila niliyekuwa nikipishana nae njiani alibaki akiwa amenitazama kwa mshang'ao.

'Mbona wananiang'alia kwa kunishang'aa'. Niliwaza nikiwa naelekea kwenye nyumba fulani, na baada ya kufika katika nyumba hiyo niliomba maji ya kunywa huku nikiwa nageuka nyuma yangu kutazama kama kuna watu ambao walikuwa wananifuata kwa muda huo.

"Kijana mbona una wasiwasi". Ilikuwa sauti ya mwanaume ambaye alionekana kuheshimika katika nyumba hiyo.

"Kuna watu wananifukuza sielewi mimi nimefanya nini?". Niliongea huku nikiwa nina mashaka makubwa sana.

"Hebu ingia ndani ili uweze kunielezea juu ya kufukuzwa na watu hao". Mwanaume huyo kwa safari hii aliongea akiwa ananishika mkono na kuniingiza ndani ila cha ajabu watu wengine walibaki wakimtazama kwa mashaka mwanaume huyo.

"Mpatieni maziwa na chakula cha kutosha maana anaonekana kutoka mbali sana".

  Mwanaume huyo baada ya kuzungumza hivyo mwanamke aliyekuwa katika sehemu hiyo aliweza kunipatia chakula na maziwa ya mtindi nilikunywa maziwa kwa haraka na hata chakula nilikula kwa harakaharaka kwa maana nilikuwa nina njaa na baada ya kumaliza kula nilimshukuru mwanaume huyo.

"Nashukuru sana kwa kile ambacho umenipatia". Niliongea nikiwa  nanawa mikono.

"Usiwe na shaka kuhusu ilo hebu nambie umepatwa na nini huko utokako?". Mwanaume huyo kwa safari hii aliongea akiwa amenitazama usoni kwangu.

  ...NINASIMULIA...

   ...Ahaa,, ni kwamba wazazi wangu na wao walikuwa hivi nilivyo mimi na nilipo wauliza kwanini hawakuwa karibu na kijiji ambacho tulikuwa karibu na sehemu hiyo tulipokuwa wanahishi mama alidai kuwa walitelekezwa na wazazi wao wakidai kuwa wao ni rahana katika kijiji hicho hivyo na mimi baada ya kunizaa na kuwa kama wao walinisihi nisije hata siku moja kwenda katika kijiji hicho kwamaana mama na baba walidai hakuna hata mwanakijiji hata mmoja ambaye alikuwa anafahamu katika sehemu hiyo tulipokuwa tunaishi baba aliweza kunifundisha kuwinda hivyo siku nyingine nilianza kwenda mwenyewe kwenye mawindo ila siku moja nikiwa nawinda katika sehemu ambayo nilikuwa nimeambiwa na baba niwinde sikuweza kuona mnyama yoyoe yule hivyo nilikiuka masharti ya baba ang'arabu yeye alinizuia kuwa nisije hata siku moja nikavuka katika sehemu hiyo.

  Ila kwa siku hiyo niliweza kukiuka kauli ya baba na pia najiraumu sana maana yote haya mimi ndo nimeyasababisha maana kipindi nikiwa natembea kwa mbali niliweza kuona watu wakiwa wanaonekana na wao kuwinda hivyo baada ya kuniona walionekana kunishang'aa.

  Mmojawapo wa wawindaji hao alinisogelea na kuniuliza jina langu niliweza kumwambia ila baada ya kumwambia jina langu mwanaume huyo aliweza kunisihi nikimbie huku akiwa anajaribu kutazama wenzake ambao walikuwa wanaonekana kunitazama na hatimae wawindaji hao walinisogelea huku wakiwa wanaonekana wazi kuwa na ushari fulani kwa jinsi sura zao zilivyokuwa!?..












ITAENDELEA...













  Usikose kipande hata kimoja cha chombezo hii kali ambayo itakuacha umepata mafunzo mbalimbali...

















Na kama ujalike page yangu unachelewa nini like page yangu inayoitwa
STORY ZA KUSISIMUA&MIKASA













'KARIBU'

2 comments:

JINSI YA KUFIKIA MALENGO YAKO

SIMULIZI FUPI YA MAISHA YANGU...    Kwa majina naitwa ISAACK KANYANKOLE,,mzaliwa wa Bukoba napenda kuwashirikisha vijana wenzangu tusitegem...