Saturday, May 12, 2018

JINSI YA KUFIKIA MALENGO YAKO

SIMULIZI FUPI YA MAISHA YANGU...

   Kwa majina naitwa ISAACK KANYANKOLE,,mzaliwa wa Bukoba napenda kuwashirikisha vijana wenzangu tusitegemee kuwaajiriwa tutegemee kujiajiri wenyewe.

   ..SOMA KWA MAKINI HUKU UKIJIFUNZA ZAIDI..

   Nakumbuka mwaka 2017 nilipata baadhi ya matatizo kwenye familia yangu sikuweza kukata tamaa ilinibidi kujikita rasmi katika tasnia ya uandishi maana niliona wazi ni sehemu ambayo ingeweza kunipatia kipato cha kujikimu mimi na familia yangu.

  Naam ilikuwa hivyo ijapokuwa kwa mara ya kwanza nilipata ugumu fulani juu ya kuuza kazi zangu ila sikuweza kukata tamaa niliendelea kuandika simulizi huku nikiamini hii ndo kazi yangu...ijapokuwa nilikuwa naandika ila kuna baadhi ya watu walikuwa wananunua mwisho wa siku niliweza kupata dili kwenye media fulani huko Bukoba nilifanya nao kazi moja na baada ya kufanya nao kazi moja ilinibidi kuandika simulizi nyingi sana.

   ...Sikuweza kukaa Bukoba kwamaana nilitaka nifanye kazi zangu ziweze kutambulika Tanzania nzima hivyo nilitafuta nauli kupitia kazi hii ya uandishi na baada ya kufanikiwa kupata nauli niliweza kuja Dar es salaam.
   Nilifikia kwa kakaangu nilikaa nae kwa miezi kama miwili na hatimae baada ya kupata pesa kupitia simulizi ilinibidi kupanga chumba changu.
   Ila baada ya kupanga chumba sikuishia hapo maana nilitaka kuwa na ofisi yangu hivyo nilikusanya pesa ambazo nilikuwa napata kupitia simulizi na kuweza kufungua ofisi yangu..

  Kupitia simulizi hii fupi nimetaka kuwaonesha vijana wenzangu kuwa kila kitu kinawezekana ukiamini wewe na hakuna ambaye ana kipaji bali kipaji kinatafutwa na wewe mwenyewe ukiamua.

    Hivyo na wewe napenda uchukue Fursa yako sasa na pia ukiwa unapenda na wewe kuwa mmojawapo wa shabiki zangu unaweza kununua simulizi zangu ambazo nauza whastup,,na hata facebook.

NA PIA MALENGO MENGINE AMBAYO NIKO NAYO MPAKA SASA NI ;
01.KUTOA VITABU
02.KUWA NA APP YANGU
03.KUWA NA ALBUM YA NYIMBO ZANGU

   NATUMAI VYOTE HIVI VITATIMIA KWAMAANA NINAAMINI NINACHOKIFANYA..HIVYO NA WEWE KIJANA MWENZANGU ANZA SASA KWA KUAMINI KUJIAJIRI NA SIO KUAJIRIWA.

  ILA KUMBUKA UKIFANYA JAMBO LOLOTE KWA KUAMINI KUNA WATU WANAONA UNACHOKIFANYA,,USIKATE TAMAA KWA KAULI ZA WAKATISHAJI TAMAA MAANA HAO WAPO ILI WEWE UFIKIE MALENGO YAKO..

SIMULIZI HII YA MAISHA YANGU UTAKUJA KUIPATA MWANZO MWISHO KUPITIA KWENYE KITABU CHANGU HIVYO USIKOSE MAANA KUNA CHANGAMOTO NYINGI AMBAZO NIMEPITIA MPAKA NILIPO SASA...

NA PIA   NAZANI UMEWEZA KUPATA SOMO KUPITIA SIMULIZI YANGU FUPI HIVYO UNAWEZA KUJIPATIA KAZI ZANGU KWA ADA NDOGO SANA ILI UWEZE KUBURUDIKA HUKU UKIJIFUNZA..

  ..KARIBU SASA..

Thursday, May 10, 2018

CHOMBEZO;KUMBE ALBINO MTAMU3&5

[5/9, 10:08 AM] Isaack kanyankole: 'CHOMBEZO YA MAPENZI'

         'INAITWA'

--KUMBE ALBINO MTAMU?.--

MTUNZI;Isaack kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;03

    ...ILIPOISHIA...

   Nilishtuka baada ya kumwagiwa maji na nilipotazama nilipokuwa sikuweza kufahamu ang'arabu niliweza kusikia minong'ono ya watu wakibishana na baada ya watu hao kubishana kwa muda mrefu na mara waliweza kuwasha taa nilipigwa na bumbuwazi baada ya kuona sehemu nilipokuwa kwa jinsi ilivyokuwa inafanana!?..

    ...ENDELEA...

   Nilistaabu sana baada ya kuona sehemu hiyo kwa jisni ilivyokuwa na nilishang'aa sana kumuona mwanaume aliyekuwa amenisaidia kuishi kwake akiwa anabishana na wavulana ambao walikuwa wameshika mapanga hama kwa hakika chumba hicho ambachjo tulikuwemo kilionekana waziwazi kuwa ni chumba cha mauaji maana chumba chote kilikuwa kimetapakaa damu na pia hata viungo vya watu vilikuwa kwenye chumba hicho na hususani viungo vya kwetu sisi albino.

''Nimesema mnipatie milionmi mbili kama si hivyo basi muache niende nae''. Mwanaume ambaye alikuwa amedai nitaishi nae aliongea huku akiwa amenitazama usoni.

''Hapana kwa dau hilo sisi hatuna labda milioni moja na laki mbili ndo tunato hivyo kubari kufanya biashara na sisi na kama ukipata mwingine tutakufanyia mpango huo wa dau unalotaka wewe''. Mmoja wa vijana ambao walikuwa wameshika mapanga aliongea akiwa anamsogelea mwanaume huyo kwa ukaribu zaidi.

''Ok sawa kwa maana ameishanitazama sura yangu hivyo nipatie pesa yangu hiyo''.

''Hoya mpatie kiasi hicho''. Na baada ya mwanaume huyo kukubari kijana mmoja aliyekuwa amenimwagia maji aliweka ndoo chini na kuelekea kwenye kisanduku fulani nja kufungua na baada ya kufungua alihesabu pesa kadhaa na baada ya kumaliza kuhesabu pesa,,pesa ambazo zilibaki alirudisha kwenye kisanduku hicho na kisha alimpatia pesa mwanaume huyo na baada ya kumaliza kumpatia mwanaume huyo pesa alinisogelea nilipokuwa na kunifungua kamba ambazo nilikuwa nimefungwa.

''Ila tambua kama niklipata mwingine pesa itakuwa ni milionmi mbili maana nyie mnapata fedha nyingi zaidi ya hapa''. Mwanaume huyo aliongea akiwa anahesabu pesa na baada ya kumaliza kuhesabu pesa hizo mwanume huyo alifunguliwa mlango wa chumba hicho na kisha alitoka huku akiwa ananipungia mkono...Nilihisi maumivu makubwa sana baada ya kuona mtu ambaye alidai kunisaidia ndo kwanza ananiuza nilisikitika sana na kujiona sina haki ya kuishi katika ulimwengu huu amabo binadamu wanaroho za wanyama wakali.

'Ina maana pesa i waliyompatia inazidi uhai wangu?'.Niliwaza nikiwa namtazama mwanaume huyo kwa jisni alivyokuwa anashuka ngazi.

''Hebu mkamateni huyo kijana na mumuweke katika sehemu ya kujinjia ila kama mnavyojua hii kazi ni ya sitri hivyo inatupasa na huyu awekwenye kwenye siri''. Kijana mmoja kati hao vijana aliongea akiwa ananisogelea nilipokuwa.

Na baada ya kuonge hivyo wavulana wawili waliweza kunisogelea na kunibeba walinipeleka mpaka kwenye sehemu fulani na kuniweka walinifunga mioguu yangu kamba na kwa jinsi walivyokuwa wananifunga nilihisi maumivu makali sana kwamaana kamba zao zilikuwa ngumu sana na kwa jinsi walivyokuwa wanazikaza ndo ziliniumiza zaidi miguu yangu na baada ya kunifunga kila mmoja alishika panga lake vema na kunyanyua juu mapigo ya moyo wangu yalinienda kwa kasi sana maana nilijua fika ndo ulikuwa mwisho wangu hivyo nilifumba macho.

''Hebu muacheni kwanza huyo tumfuate huyu mwanaume kabla ajafika mbali kwamaana kama mnavyojua hii ni siri hivyo ikigundulika tu lazima tutafukuzwa katika kijiji hiki na kama mnavyojua kazi ambazo zimetuleta katika kijiji hiki ni nyingi sana''. Ilikuwa ni sauti ambayo ilitoka kwa mwanaume ambaye alikuwa pembeni yangu.
   Na kweli baada ya mvulana huyo kusema hivyo kila mtu aliweza kushusha panga lake na kutoka nje kwa haraka na baada ya wote kutooka nje nilimshuru sana Mungu baada ya kuona nim,ewweza kupona kwenye kisanga hicho ambacho kilikuwa mbele yangu. Na bada ya kuniacha katika sehemu hiyo nilianza kutazama ni jinsi gani ningeweza kujinasua katika sehemu hiyo.

Na kilichoweza kunisaidia zaidi hawakuwa wamenifunga mikono hivyo niliweza kujivuta kwa kutumia mikono na kushika panga ambalo lilikuwa kando yangu na kukata kamba ambazo zilikuwa zimenifunga na baada ya kumaliza kuzifungua kamba hhizo nilienda mpaka kwenye kisanduku ambacho niliweza kuona wakihifadhi pesa na kuchukua kiasi chote cha fedha iliyokuwemo sikuweza kuzihesabu kwamaana zilikuwa ni nyingi sana hivyo nilizifunga kwenye shati ambalo lilikuwa kando na kifurushi hicho na kisha nilitoka katika chumba hicho huku nikiwa naang'aza macho yangu huku na kule kwa hofu kubwa sana. Nilipiga hatua za kunyata huku nikiwa natazama kwa umakini kila sehemu ila kipindi nikiwa nimetoka katika chumba hicho nikiwa kwenye kichaka fulani huku nikiwa nachungulia niliweza kumuona mwanaume ambaye alikuwa ameniuza akiwa amekatwa mguu na pia mikono nilihisi mwili wangu kupigwa na ubaridi baada ya kuona kijana mmoja akinyanyua upanga kwa juu na kisha kufyeka shingo yake.

''Mamaaaaaa....?'. Kelele hiyo ilinitoka huku nikiwa nakimbia baada ya kuona tukio hilo.

Na kwa nyuma yangu niliweza kusikia watu wakiwa wananikimbiza nilikimbia na hatimae niliweza kufika kwenye korongo na nilipogeuka nyuma na kutazama niliweza kuona vichaka vikiwa vinatikisika kuashiria kulikuwa kuna watu wanakuja nilipokuiwa.

  Uwoga nao ulinitawala zaidi kila nilivyokuwa nikitazama kwenye korongo ilo kwamaana lilikuwa lefu kwelikweli hofu ilizidi zaidi baada ya kuona wazi nakaribiwa kufikiwa na sikuwa na sehemu nyingine ambayo ningeweza kupita zaidi ya kuirudi nyuma. Sikufahanmu ujasiri niliupata wapi wa kuruka kwenye korongo hilo na baada ya kuruka nilienda najiviringisha huku nikiwa najipiga kwenye mawe na pia nilichomwa na miiba na hatimae nilikwama katika sehemu fulani?..











ITAENDELEA








































Usikose kipande hata kimoja cha chombezo hii kali ambayo itakuacha umepata mafunzo mbalimbali...


















Na kama ujalike page yangu unachelewa nini like page yangu inayoitwa
STORY ZA KUSISIMUA&MIKASA

















'KARIBU'
[5/9, 10:17 AM] Isaack kanyankole: 'CHOMBEZO YA MAPENZI'

       'INAITWA'

--KUMBE ALBINO MTAMU?.--

MTUNZI;Isaack Kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;04

....ILIPOISHIA...

Sikufahamu ujasiri niliupata wapi wa kuruka kwenye korongo hilo na baada ya kuruka nilienda najiviringisha huku nikiwa najipiga kwenye mawe na pia nilichomwa na miiba na hatimae nilikwama katika sehemu fulani?..

   ...ENDELEA...

Nilijaribu kujinasua katika sehemu hiyo kwamaana nilikuwa nimebanwa mkono na baada ya kufanya juhudi kwa muda mrefu ya kuweza kujinasua katika sehemu nilifanikiwa na baada ya kunasua katika sehemu hiyo nilishika majani kwa nguvu na kuanza kushuka kwa taratibu na hatimae niliweza kufika chini.

Baada ya kufika chini ilinibidi nijitazame shati ambalo nilikuwa nimejifunga kiunoni nilifarijika sana baada ya kuona lipo hivyo ilinibidi nijifungue na kutazama kwa kile ambacho nilikuwa nimekiweka kama kilikuwemo nilifungua huku uwoga ukinitawala sana juu ya pilika ambazo nilikuwa nimezipata kipindi naserereka kutoka juu ya korongo hilo.

''Asante Mungu?''. Niliongea pekeangu huku nikiwa natazama pesa ambazo zilikuwa kwenye shati hilo na baada ya kuakikisha zipo nilijifunga tena na kuanza safari ila kwasafari hii nilianza kuhisi maumivu kwenye mwili wangu hivyo iulinibidi kukaa chini.

Kila sehemu ya mwili wangu nilihisi maumivu makali sana hususani kwenye kichwa na pia hata kwenye mikono na miguu damu zilikuwa zimetapaaka kwenye miguu yangu. Maumivu yalivyozidi ilinibidi kujilaza katika sehemu hiyo na baada ya kujilaza nilipitiwa na usingizi nilikuja kushtuka baada ya kusikia mngurumo wa gari.

Hivyo niliamka kwa haraka na kusimama nilianza kutembea kufuata mngurumo huo wa gari ambao niliweza kuhusikia na baada ya kutembea huku nikiwa najivuta kwamaana bado nilikuwa nasikia maumivu makali sana kwenye viungo vya mwili wangu , na baada ya kuona jani la mti fulani ilinibidi nilisogelee huku nikiwa nachechemea kwa kujivuta.

Nilichuma tawi hilo na kulitafuna na kisha nilillitema na baada ya kumaliza kulitema nililishika na kuanza kujipaka kila sehemu ya kiungo changu ambacho nilihisi maumivu makalia sana maana tawi ilo lilikuwa linapunguza makali ya maumivu hayo.

Na baada ya kumaliza kujipaka majani hayo maumivu ambayo nilikuwa nayasikia yaliweza kupungua hivyo nilisimama na kuendelea kufatilia mlio huo wa gari nilipokuwa nausikia nilitembea huku nikiwa najivuta na hatimae niliweza kufanikiwa kuona katika sehemu gari hilo lilipokuwa. Na katika sehemu hiyo niliweza kuona wanaume wakiwa wamesimama na vijana wengine walikuwa wakionekana kubeba vitu na kuviweka kwenye gari hilo na kwa jinsi nilivyokazia macho kutazama walikuwa wanabeba nini niliweza kufanikiwa kuona walichokuwa wanabeba vijana ha,,walionekana wakiwa wanabeba mbao na kuziweka kwenye gari hilo.

Baada ya kuona watu hao wakiwa wanaendelea kubeba mbao ilinibidi kuendelea kutembea kuwasogel;ea watu hao ila kipindi nikiwa naendelea kutembea nafsi yasngu iligoma kuwafuata watu hao na kipindi nikiwa natembea niliweza kuona kinjia kingine hivyo ilinibidi nifuate uamuzi wa nafsi yangu na kufuata kinjia hicho.
  Nilitembea na hatimae niliweza kufika kwenye makazi ya watu kila mtu niliyekuwa napishana nae alionekana kunishang'aa kwa jinsi nilivyokuwa sikujali hilo nilitembea mpaka nilipofika mgahawa fulani na baada ya kufika kwenye mgahawa huo niliagiza chakula na baada ya kuletewa chakula nilikula kwa haraka kwa jinsi nilivyokuwa na njaa.

Na niliposhiba nilimpatia pesa muhudumu huyo huku nikiwa namtazama usoni kwamaana alionekana kunishang'aa kwa jinsi nilivyokuwa nakula kwa haraka, ''Samahani kaka kwani wewe unatoka wapi?". Muhudumu huyo aliniuliza huku akiwa ananipatia chenji.

''Ni vitu vingi ambavyo vimenisibu ila kama hautojari naomba unielekeze duka la nguo lilipo na pia kama unaweza kunisaidia kupata chumba kwasasa utakuwa umenisaidia''. Nilizungumza nikiwa napokea chenji huku nikiwa nimemtazama binti huyo.

''Dah chumba siwezi kujua kilipo ila unaweza kwenda unaulizia na pia duka la nguo ambalo unahitaji la nguo liko hapo mbele yaani duka ambalo limetazama kwenye mgahawa wetu''.

''Sawa nashukuru sana''.

Nilinyanyuka na kisha nilianza kupiga hatua ya kuelekea kwenye duka la nguo ila kipindi nikiwa natoka kwenye mgahawa huo niliweza kuteleza na kudondoka na baada ya kudondoka kila mtu alinitazama nilipigwa na butwa baada ya kuona watu hao wakiwa wamenikazia macho?...



















ITAENDELEA..
















   Usikose kipande hata kimoja cha chombezo hii kali ambayo itakuacha umepata mafunzo mbalimbali...
















Na kama ujalike page yangu unachelewa nini like page yangu inayoitwa
STORY ZA KUSISIMUA&MIKASA














'KARIBU'
[5/9, 10:18 AM] Isaack kanyankole: 'CHOMBEZO YA MAPENZI'

       'INAITWA'

--KUMBE ALBINO MTAMU?.--

MTUNZI;Isaack Kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;05

     ...ILIPOISHIA...

Nilinyanyiuka na kisha nilianza kupiga hatua ya kueleka kwenye duka la nguo ila kipindi nikiwa natoka kwenye mgahawa huo niliweza kuteleza na kudondoka na baada ya kudondoka kila mtu alinitazama nilipigwa na butwaa baada ya kuona watu hao wakiwa wamenikazia macho?...

    ...ENDELEA...

Na nilipotazama kando yangu niliweza kuona pesa ambazo nilikuwa nazo zikiwa zimemwagika chini hivyo ilinibidi kuokota,,ila kipindi nilivyokuwa nikiokota watu ambao walikuwa kwenye mgahawa huo walionekana kunitazama kwa umakini wa hali ya juu sana.

  Na mimi ilinibidi kutowafatilia hivyo niliokota pesa hizo na baada ya kumaliza kuokota pesa hizo ilinibidi kuzifunga vema kwenye shati na kisha nilielekea kwenye duka la nguo na baada ya kufika kwenye duka la nguo nilianza kutazama nguo ambazo niliona zingenifaa kuvaa.

"Nahitaji hizi nguo sh ngapi?". Niliuliza huku nikiwa nimemtazama muuzaji huyo aliyeonekana kuwa na mashaka na mimi kwa jinsi nilivyokuwa.

"Aha,,,sh elfu hamsini hizo zote".

"Oho,,sawa". Niliitikia huku nikitoa pesa na kuanza kuhesabu na baada ya kufika kiasi cha shilingi elfu hamsini nilimkabidhi kijana huyo.

"Hebu leta nikuwekee kwenye mfuko".

"Niwekee hizi harafu kuhusu hizi nataka kuvaa".

"Ohoo sawa sehemu ya kuvalia ni hapo mbele kidogo na kona". Muuzaji huyo aliongea akiwa ananionesha sehemu hiyo.

"Nimeona". Niliitikia huku nikipiga hatua za kuelekea sehemu ambayo nilikuwa nimeoneshwa.

Na baada ya kufika katika sehemu hiyo niliweza kubadilisha nguo na pesa zangu ilinibidi kuzifunga kwenye nguo ambazo nilikuwa nimezivua,,na baada ya kumaliza kuvaa nilienda moja kwa moja mpaka kwa muuzaji huyo.

"Hivyo unauza shilingi ngapi?".

"Hayo mabegi nauza elfu ishirini".

"Hebu nipatie hilo begi". Nilizungumza nikiwa nachomoa elfu ishirini na kumpatia.

  Na baada ya kuona nimepata begi ilinibidi kuweka pesa zangu kwenye begi na pia hata nguo nyingine ambazo nilikuwa nazo,,nilitoka kwenye duka hilo la nguo huku nikiwa nina mawazo mengi sana kichwani niliwaza ningeenda wapi na pia sikufahamu hapo nilipokuwa ni wapi hivyo ilinibidi kumuuliza mtu ambaye alikuwa anaonekana kunitazama kipindi nilivyokuwa natembea.

"Shikamoo,,samahani kwa usumbufu". Nilizungumza nikiwa namtazama mwanaume huyo usoni kwamaana alionekana kunitazama sana.

"Marahaba bila samahani".

"Nilikuwa naulizia hapa ni wapi maana kuna watu ambao tulikuwa tumepanga kuonana lakini siwaoni?". Ilinibidi nimdanganye mwanaume huyo ili niweze kufanikiwa juu ya azima yangu.

"Dah,,pole sana hapa ni Geita vijijini na pia sehemu hii ni hatari sana kwa jinsi ulivyo hivyo fanya haraka kabla ya giza kuzama uwe umetoweka katika kijiji hiki kwamaana hapa kuna watu wabaya sana,,,na inawezekana watu ambao ulikuwa umepanga nao kuja kuonana katika sehemu hii wameishakuuza hivyo nakushauri fanya haraka uondoke katika kijiji hiki". Mwanaume huyo aliongea akiwa anaonekana waziwazi kunisisitizia juu ya suala la kuondoka.

"Sasa sifahamu hata barabaraba ilipo?". Niliongea huku nikiwa nina mashaka juu ya mambo ambayo alikuwa amenambia mwanaume huyo maana hata mapigo ya moyo wangu yalianza kunienda kwa kasi sana juu.

"Unaona kibarabara hiki nyoosha nacho ila jitahidi sana kukimbia maana giza likitanda tu sizani kama utaweza kupona maana sehemu hii hususani watu ambao hawafahamiki uwa wanahua watu na pia hususani kama nyie uwa wanawachinja na viungo vyenu wanaenda kuviuza". Mwanaume huyo alizungumza akiwa ananivuta kando na pia akijaribu kuninyooshea kidole katika sehemu fulani.

"Unaona watu kama hao".

"Ndio nawaona". Nilijibu huku nikiwa ninatetemeka juu ya maneno ambayo nilikuwa nimeambiwa na mwanaune huyo.

"Basi kama umeweza kuwaona watu hao wanasadikika kuua watu hivyo fanya haraka".

  Na kweli watu hao kwa jinsi walivyokuwa walifanana kama majambazi maana walikuwa wamevaa miwani mieusi na pia makoti marefu,,sikuweza kumuaga mwanaume huyo hivyo nilichoropoka kwenye mikono yake na kuanza kukimbia baada ya kuona mmoja kati ya hao watu aliokuwa amenionesha kugeuka na kutazama sehemu niliyokuwepo mimi..nilikimbia kufuata kibarabara ambacho mwanaume huyo alichokuwa amenambia nilikimbia ila kipindi nikiwa nakimbia na mara kwa nyuma yangu niliweza kusikia mlio wa kitu fulani kiking'uruma hivyo nilisimama na kugeuka nyuma.

"Unaelekea wapi?". Niliuliza huku nikiwa namkibilia kijana huyo aliyekuwa na pikipiki.

"Naelekea mjini".

"Unaweza kunipeleka".

"Panda twende ila nauli ni shilingi elfu kumi na tano". Kijana huyo alizungumza akiwa anawasha pikipiki.

"Sawa amna shida". Nilizungumza huku nikiwa namuomba Mungu aweze kuniepusha na kisanga ambacho kilikuwa mbele yangu.

  Na kweli safari ilianza na kwa jinsi barabara ilivyokuwa mbaya niliona wazi kama tulikiwa atuendi niliona kana kwamba tunasogea taratiibu sana,,kijana huyo nae alionekana kuogopa kwamaana alikuwa akitazama saa kila muda.
   Na hatimae pikipiki ilizima kabisa kijana huyo alijaribu kuwasha lakini pikipiki haikuwaka ang'arabu iliwasha taa tu.

"Dah sehemu hii ni hatari sana hebu shuka kwanza niishtue kwanza pikipiki".

"Sawa fanya haraka basi". Nilizungumza nikiwa nashuka huku nikiwa nina mashaka makubwa sana juu ya sehemu hiyo na pia giza lilikuwa limeanza kutanda kwenye anga.

Na baada ya kushuka nilianza kuang'aza huku na kule huku nikiwa namsihi kijana huyo aweze kutengeneza haraka pikipiki yake...ila cha ajabu pikipiki ilivyowaka tu kijana huyo aliweza kukimbiza pikipiki yake na kuniacha katika pori hilo uwoga ulinitawala zaidi ya mara ya kwanza.

   Na sehemu hiyo nilipokuwa nilianza kusikia michakacho ya watu wakiwa wanaongea na huku wakiwa wanakuja nilipokuwa nimesimama miguu yangu ilianza kutetemeka kila nilivyokuwa nikikumbuka kauli za mwanaume ambazo alikuwa amenambia!?...











ITAENDELEA....















  Usikose kipande hata kimoja cha chombezo hii kali ambayo itakuacha umepata mafunzo....






















Na kama ujalike page yangu unachelewa nini like page yangu inayoitwa
STORY ZA KUSISIMUA&MIKASA













'KARIBU'

CHOMBEZO;KUMBE ALBINO MTAMU 2

'CHOMBEZO YA MAPENZI'

      'INAITWA'

--KUMBE ALBINO MTAMU?.--

MTUNZI;Isaack Kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;02

    ...ILIPOISHIA...

Mmojawapo wa wawindaji hao alinisogelea na kuniuliza jina langu niliweza kumwabia ila baada ya kumwambia jina langu mwanaume huyo aliweza kunisihi nikimbie huku akiwa anajaribu kutazama wenzake ambao walikuwa wanaonekana kunitazama na hatimae wawindaji hao walinisogelea huku wakiwa wanaonekana wazi kuwa na ushari fulani kwa jinsi sura zao zilivyokuwa!?..

     ...ENDELEA...

Na kweli kwa jinsi nilivyokuwa nawakisia ilikuwa hivyo kwa maana wawindaji hao walianza kunikimbiza huku wakiwa wanajaribu kunitisha kwa maneno ya ukali ila sikuweza kusimama nilikimbia mpaka tulipokuwa tunaishi.
   Sikufahamu kama  nilikuwa nimefanya kosa kwamaana niliweza kushuhudia wazazi wangu wakikatwakatwa viungo vyao na watu hao kwa jinsi walivyokuwa wakikata viungo vya wazazi wangu walionekana kushangilia na baada ya watu hao kumaliza kukatakata miili ya wazazi wangu mmoja wa wawindaji aliweza kuwazuia wawindaji hao huku akijaribu kuwazuia kuwa siku nyingine ndo wataweza kufanya dhamira ya kunikatakata.

    Hivyo baada ya wauaji hao kuelezewa na mwanaume huyo ambaye alionekana waziwazi kutokubalina juu ya jambo ambalo walikuwa wamefanya la kuua wazazi wangu.
    Mwanaume huyo aliweza kunifunga kamba na kisha aliweza kunipatia kidonge fulani alinisisitiza kuwa nikimeze na kweli niliweza kumeza kidonge hicho na baada ya kukimeza kidonge sikuelewa ni nini ambacho kiliendelea baada ya kujikuta nikiwa mgongoni mwa mwanaume huyo akiwa anakimbia.

   Na baada ya kuzungumza mwanaume huyo aliweza kunishusha chini na kufurahia ila kipindi akiwa anajaribu kutaka kunisimulia maana mambo ambayo yalikuwa yamenitokea niliona kama yalikuwa kama ndoto ila kwa mbali na sehemu tulipokuwa tuliweza kusikia michakacho ya watu wakiwa wanakuja tulipokuwa mwanaume huyo alinibeba tena mgongoni na kuanza kukimbia ila kipindi akiwa anakimbia aliweza kujikwaa na kudondoka chini na baada ya kudondoka chini mwanaume huyo akuweza kuendelea kukimbia alidai kuwa nikimbie nilijaribu kumsihi lakini hakuweza kunyanyuka hivyo nilimuacha na baada ya kumuacha nilianza kukimbia mpaka nafika katika kijiji chenu.

"Dah,,pole sana inatupasa kukupeleka kwa kiongozi wa kijiji hiki ili uweze kuishi hapa maana kijiji hiki hususani ni kijiji cha watu wakarimu sizani kama mkuu wetu hatakataa". Mwanaume huyo aliongea akiwa anasimama na kunishika mkono.
   Niliongozana nae mpaka kwenye nyumba ambayo ilikuwa imejengwa kwa tofali na pia ilikuwa imeezekwa kwa mabati tulisimama kwa nje, mwanaume ambaye alikuwa amenileta katika sehemu hiyo aliingia ndani hakuchukua muda mwingi alitoka ndani akiwa ameongozana na mwanaume ambaye alionekana wazi kuwa na umri kuanzia miaka kama tisini hivi ila cha ajabu alikuwa anatembea vema tu.

   Kiongozi huyo baada ya kutoka nje aliweza kunitazama usoni kana kwamba anaonekana kunitafakari juu ya jinsi nilivyokuwa na pia mwanaume ambaye alikuwa amenileta katika sehemu hiyo alionekana kumuelezea juu kisa changu.

"Nazani kijiji hiki ni cha ukarimu hivyo nataka ambaye atahishi na huyu kijana?". Kiongozi huyo aliongea akiwa  anasimama mbele ya wanakijiji ambao walikuwa wamezingira katika sehemu hiyo.

Hakuna hata mmoja ambaye aliweza kuzungumza kila mtu alibaki kimya huku wengi wao wakionekana kunishang'aa kwa jinsi nilivyokuwa. "Nitaishi nae mimi". Ilikuwa ni sauti ya mwanaume ambaye alikuwa amenileta katika sehemu hiyo alizungumza akiwa ananisogelea nilipokuwa na kunishika mkono.

Kila mtu aliyekuwa katika sehemu hiyo alipiga makofi na hatimae nilipelekwa kwa kiongozi huyo wa kijiji hicho kiongozi huyo aliongea maneno fulani ambayo sikuelewa alikuwa ana maana gani?, na baada ya kumaliza kuongea aliweza kuniruhusu kusimama.

   Kila mtu aliyekuwa katika sehemu hiyo aliweza kuondoka hivyo na mimi niliongozana na mwanaume huyo nilienda nae mpaka kwake nilioneshwa chumba ambacho ningetumia kulala. Na siku iliyofuata niliamka mapema na kusafisha uwanja na baada ya kumaliza kusafisha uwanja nilienda moja kwa moja mtoni kwamaana niliweza kufahamu ulipokuwa ila baada ya kufika mtoni niliweza kukuta wanaume fulani wakiwa mtoni na walikuwa wameshika mapanga.
   Niliteka maji huku nikiwa natetemeka na baada ya kumaliza kuteka maji nilibeba vifaa vyangu ila kitendo cha kupiga hatua kama mbili hivi wanaume hao walinizunguka huku wakiwa wameweka vidole vyao kinywani mwao kuashilia nisipige kelele.

"Ukijaribu kupiga kelele tunakuua hivyo kaa kimya". Kijana mmoja aliongea huku akiwa ananisogelea nilipokuwa na baada ya kunisogelea nilizibwa na kitambaa usoni sikufahamu kilichoendelea maana baada ya kuniweka kitambaa usoni nilihisi macho yangu kuwa mazito.

   Nilishtuka baada ya kumwagiwa maji na nilipotazama nilipokuwa sikuweza kufahamu ang'arabu niliweza kusikia minong'ono ya watu wakibishana na baada ya watu hao kubishana kwa muda mrefu na mara waliweza kuwasha taa nilipigwa na bumbuwazi baada ya kuona sehemu nilipokuwa kwa jinsi ilivyokuwa inafanana!?...

 


















ITAENDELEA...


















  Usikose kipande hata kimoja cha chombezo hii kali ambayo itakuacha umepata mafunzo mbalimbali...















Na kama ujalike page yangu unachelewa nini like page yangu inayoitwa
STORY ZA KUSISIMUA&MIKASA











'KARIBU'

CHOMBEZO; KUMBE ALBINO MTAMU

'CHOMBEZO YA MAPENZI'

     'INAITWA'

---KUMBE ALBINO MTAMU?.---

MTUNZI;Isaack Kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;01

     ...UTANGULIZI...

Hii ni chombezo ambayo imesukwa vema hivyo soma kwa umakini huku ukijifunza maana mambo ambayo utakuta katika chombezo hii yatakuacha umepata funzo kubwa sana.. Mtunzi wa chombezo hii anashauri kwa ambaye atasoma chombezo hii awe na umri wa kuanzia miaka 18+ maana kuna mambo ambayo yatakuacha ukiwa hoi taabani,,na pia tuepukane na mila potofu katika jamii ambazo tunaishi. Soma kisha ujifunze.

    ...ANZA NAYO...

  Radi na mingurumo zilisikika kwa mbali sana,,kwamaana nilikuwa nimebebwa mgongoni na mtu aliyekuwa amenibeba alikimbia kwa kasi sana. Hivyo sikuwa nasikia vema mtu huyo aliendelea kukimbia na kila alivyokuwa anakimbia niliweza kukumbuka matukio ambayo yalikuwa yamenitokea kwa muda mfupi uliokuwa umepita.

"Niachie mimi". Nilizungumza kwa ukali sana huku nikijaribu kuleta purukushani za hapa na pale maana nilikuwa nina hofu kubwa sana juu ya mambo ambayo yalikuwa yamenikuta kwa kipindi kifupi.

  Na kweli baada ya kufanya purukushani za hapa na pale mtu huyo aliweza kunishusha huku akiwa anaonekana kutoamini. "Pole sana David". Mtu huyo aliongea akiwa ananitoa mgongoni kwake.

"Mama na baba wako wapi?". Niliuliza huku nikiwa nimemtazama mtu huyo ambaye sikuwa namfahamu.

"Wazazi wako wameuwawa kwa kuchinjwa na mapanga na hapa unatafutwa na watu hao wabaya". Kijana huyo aliongea akiwa  amenitazama usoni kana kwamba anafikiri kwa ambacho nitakifanya.

  Ila kipindi hichohicho kwa mbali tuliweza kusikia watu wakija tulipokuwa hivyo kijana huyo alinibeba tena na kuanza kukimbia ila kipindi akiwa anakimbia na mara aliweza kuteleza na kudondoka.

"David kimbia watu hao ni wabaya watakuua kimbia niache maana siwezi kuendelea na safari nendaaa". Kijana huyo alisinisitiza huku akiwa ameshika mguu wake.

"Amka twende watakuua hao watu?". Nilizungumza nikiwa najaribu kumnyanya kijana huyo lakini alikataa katukatu na kudai asingeweza kuendelea na safari hivyo alinisisitiza niendelee kukimbia.

   Ilinibidi kumuacha kijana huyo na kuendelea kukimbia nilikimbia huku nikiwa nageuka nyuma na kutazama kama watu hao walikuwa wananikimbiza ila sikuweza kumuona mtu yoyote yule ang'arabu niliweza kusikia sauti ya mtu akipiga kelele ya kuomba msaada.

'Ina maana kile ambacho nilikuwa nakiota ni kweli'. Niliwaza nikiwa naendelea kupanda mlima.

  Na baada ya kumaliza kupanda kilele hicho cha mlima kwa mbali na sehemu hiyo niliweza kufanikiwa kuona watu wakiwa wanafanya shughuli za hapa na pale hivyo nilianza kutembea kuelekea katika kijiji hicho nilitembea takribani masaa mawili na jua lilipokuwa kali sana ilinibidi kwenda kwenye kivuli maana nilihisi kuungua kwa ngozi yangu.
Na baada ya jua kuzama niliendelea na safari mpaka kwenye kijiji hicho naam baada ya kufika katika kijiji hicho ila kila niliyekuwa nikipishana nae njiani alibaki akiwa amenitazama kwa mshang'ao.

'Mbona wananiang'alia kwa kunishang'aa'. Niliwaza nikiwa naelekea kwenye nyumba fulani, na baada ya kufika katika nyumba hiyo niliomba maji ya kunywa huku nikiwa nageuka nyuma yangu kutazama kama kuna watu ambao walikuwa wananifuata kwa muda huo.

"Kijana mbona una wasiwasi". Ilikuwa sauti ya mwanaume ambaye alionekana kuheshimika katika nyumba hiyo.

"Kuna watu wananifukuza sielewi mimi nimefanya nini?". Niliongea huku nikiwa nina mashaka makubwa sana.

"Hebu ingia ndani ili uweze kunielezea juu ya kufukuzwa na watu hao". Mwanaume huyo kwa safari hii aliongea akiwa ananishika mkono na kuniingiza ndani ila cha ajabu watu wengine walibaki wakimtazama kwa mashaka mwanaume huyo.

"Mpatieni maziwa na chakula cha kutosha maana anaonekana kutoka mbali sana".

  Mwanaume huyo baada ya kuzungumza hivyo mwanamke aliyekuwa katika sehemu hiyo aliweza kunipatia chakula na maziwa ya mtindi nilikunywa maziwa kwa haraka na hata chakula nilikula kwa harakaharaka kwa maana nilikuwa nina njaa na baada ya kumaliza kula nilimshukuru mwanaume huyo.

"Nashukuru sana kwa kile ambacho umenipatia". Niliongea nikiwa  nanawa mikono.

"Usiwe na shaka kuhusu ilo hebu nambie umepatwa na nini huko utokako?". Mwanaume huyo kwa safari hii aliongea akiwa amenitazama usoni kwangu.

  ...NINASIMULIA...

   ...Ahaa,, ni kwamba wazazi wangu na wao walikuwa hivi nilivyo mimi na nilipo wauliza kwanini hawakuwa karibu na kijiji ambacho tulikuwa karibu na sehemu hiyo tulipokuwa wanahishi mama alidai kuwa walitelekezwa na wazazi wao wakidai kuwa wao ni rahana katika kijiji hicho hivyo na mimi baada ya kunizaa na kuwa kama wao walinisihi nisije hata siku moja kwenda katika kijiji hicho kwamaana mama na baba walidai hakuna hata mwanakijiji hata mmoja ambaye alikuwa anafahamu katika sehemu hiyo tulipokuwa tunaishi baba aliweza kunifundisha kuwinda hivyo siku nyingine nilianza kwenda mwenyewe kwenye mawindo ila siku moja nikiwa nawinda katika sehemu ambayo nilikuwa nimeambiwa na baba niwinde sikuweza kuona mnyama yoyoe yule hivyo nilikiuka masharti ya baba ang'arabu yeye alinizuia kuwa nisije hata siku moja nikavuka katika sehemu hiyo.

  Ila kwa siku hiyo niliweza kukiuka kauli ya baba na pia najiraumu sana maana yote haya mimi ndo nimeyasababisha maana kipindi nikiwa natembea kwa mbali niliweza kuona watu wakiwa wanaonekana na wao kuwinda hivyo baada ya kuniona walionekana kunishang'aa.

  Mmojawapo wa wawindaji hao alinisogelea na kuniuliza jina langu niliweza kumwambia ila baada ya kumwambia jina langu mwanaume huyo aliweza kunisihi nikimbie huku akiwa anajaribu kutazama wenzake ambao walikuwa wanaonekana kunitazama na hatimae wawindaji hao walinisogelea huku wakiwa wanaonekana wazi kuwa na ushari fulani kwa jinsi sura zao zilivyokuwa!?..












ITAENDELEA...













  Usikose kipande hata kimoja cha chombezo hii kali ambayo itakuacha umepata mafunzo mbalimbali...

















Na kama ujalike page yangu unachelewa nini like page yangu inayoitwa
STORY ZA KUSISIMUA&MIKASA













'KARIBU'

JINSI YA KUFIKIA MALENGO YAKO

SIMULIZI FUPI YA MAISHA YANGU...    Kwa majina naitwa ISAACK KANYANKOLE,,mzaliwa wa Bukoba napenda kuwashirikisha vijana wenzangu tusitegem...